Wanafunzi Bora wazungumzia matokeo - The Best Schools In Tanzania
Headlines News :
Home » » Wanafunzi Bora wazungumzia matokeo

Wanafunzi Bora wazungumzia matokeo

Written By mahamoud on Thursday 20 March 2014 | 04:51

SAID JUMA IRANDO
Dar es Salaam. Mwanafunzi bora wa kwanza kitaifa katika matokeo yaliyorekebishwa ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka 2012, Said Irando kutoka Shule ya Sekondari Feza ya jijini Dar es Salaam, ameeleza kushangazwa na matokeo hayo kwa kuwa hakuyatarajia.
Mwanafunzi huyo ambaye tayari ameshaanza masomo ya Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Feza, alisema kuwa ingawa alisoma kwa bidii lakini hakudhani kama angeweza kushika nafasi ya kwanza kitaifa na kwamba anamini mafanikio yake kitaaluma yana ‘mkono wa Mungu’.
“Sikutegemea kabisa kuwa mwanafunzi bora, ingawa nilisoma kwa bidii kubwa nia yangu ilikuwa ni kutaka kufaulu tu; Ni Mungu amenisaidia,” alisema Irando.
Alisema kujituma katika masomo, mazingira mazuri ya kusomea na upatikanaji wa vifaa muhimu vya kujifunzia ndiyo yaliyomwezesha kusoma na kufanya vizuri.
Irando ambaye ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto watatu, alisema kurekebishwa kwa matokeo ya kidato cha nne kulibadilisha alama za matokeo yake kutoka Daraja la kwanza akiwa na alama tisa hadi saba, zilizomfanya kuwa mwanafunzi bora kitaifa na mwafunzi bora wa kwanza kati ya wavulana kumi bora pia kitaifa.
Mwanafunzi huyo alibainisha kuwa pamoja na wazazi wake kuwa ni wafanyabiashara, yeye anatamani kuwa mhandisi ingawa bado hajajua atakuwa mhandisi katika tasnia gani.
“Natamani sana kuwa mhandisi hiyo ndiyo ndoto yangu ingawa bado sijajua nitakuwa mhandisi wa sekta gani,” alisema Irando.
Irando alisoma elimu ya msingi katika Shule ya Msingi J.K Nyerere ambako alifaulu na kuchaguliwa kujiunga na Sekondari Pugu, lakini wazazi wake waliamua kumpeleka Shule ya Sekondari Feza.
Naye mwanafunzi Joshua Azza kutoka Sekondari ya Wavulana Marian ambaye ameshika nafasi ya saba kitaifa kati ya wanafunzi kumi bora baada ya kupata daraja la kwanza akiwa na alama 11, alisema ameyapokea matokeo hayo kwa furaha akiamini atatimiza lengo lake la kuwa daktari wa upasuaji.
“Natarajia kuwa daktari wa upasuaji, kwa matokeo haya nadhani nitafanikiwa,” alisema Azza ambaye wazazi wake wote ni walimu alipozungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Saidi Nchimbi kutoka Sekondari ya Feza, ambaye ameshika nafasi ya nane kati ya wanafunzi kumi bora kitaifa, alisema kuwa siku zote alikuwa akisoma kwa uwezo wake wote na kwamba alikuwa akitamani kufaulu kwenye mitihani yake yote aliyopewa.
Nchimbi amefanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kupata daraja la kwanza akiwa na alama nane. Katika matokeo ya awali mwanafunzi huyo alikuwa na alama 11.
“Malengo yangu natamani siku moja niwe mhandisi wa majengo,” alisema Nchimbi.
Wakati huohuo, mwanafunzi aliyeshika nafasi ya tatu kati ya wanafunzi watano bora kwenye masomo ya Sayansi katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2012 yaliyotangazwa jana, Gasper Mung’ong’o amesema kuwa Mungu ndiyo alimwezesha kupata matokeo mazuri kwani alikuwa akimwomba sana.
“Mungu ndiye aliyenifanikisha kupata matokeo haya na kushika nafsi ya tatu, nilikuwa nikimwomba sana, “ alisema Mung’ong’o na kuongeza kuwa: Nilikuwa na ratiba ya kusali kila siku kabla ya kwenda kulala ili niweze kufaulu masomo yangu.
Share this article :

1 comment:

  1. The Best Casino Slots - Mapyro
    New and used slot machines & free spins in 성남 출장마사지 2021 The best casino 화성 출장마사지 slot games at Mapyro. Find 속초 출장안마 top slots, 거제 출장샵 top tables, 서울특별 출장마사지 & more!

    ReplyDelete

 
Copyright © 2014. The Best Schools In Tanzania - All Rights Reserved
Design by Bongotech